IFAHAMU VPN NI NINI ?
VPN ni Nini? 🔎 VPN ni kifupi cha Virtual Private Network (Mtandao Binafsi Fikizi). Ili kuelewa kirahisi, hebu tutumie mfano huu : Fikiria unamtumia rafiki yako barua ambayo unahitaji ibaki siri kati yenu wawili. Badala ya kuiweka kwenye bahasha ya kawaida, unaamua kuiweka kwenye sanduku maalum la siri (au kuandika ujumbe kwa lugha ya siri/kodi) ambayo wewe na rafiki yako pekee ndiyo mnaweza kuufungua au kuuelewa. VPN ni sawa na hicho sanduku maalum la siri au lugha ya siri unayotumia mtandaoni. Inakuwezesha kupata usalama na usiri unapowasiliana na mtu au unapotumia intaneti kupitia kompyuta au kifaa chako. VPN INAFANYAJE KAZI? Ili mtandao wa VPN ufanye kazi kuna vitu vinne vinahitajika, Ambavyo ni KIFAA CHAKO, VPN SEVA, TUNNEL na INTERNET. 1) KIFAA CHAKO Hii ndiyo sehemu ambayo ujumbe unatengenezwa kwa ajili ya kutuma, Kwa maana ya mtu wa kwanza na ninapo sema KIFAA CHAKO, Hapa namaanisha inawez...